Jumapili, Januari 11, 2015

Mbunge wa mbeya mjini Mr sugu akiwa na rafiki yake kando ya gari lao baada ya kupinduka katika mteremko wa kitonga leo.



Mbunge wa jimbo la Mbeya mjini Joseph mbilinyi a.k.a Mr Sugu kupitia chama ca demokrasia na Maendeleo [CHADEMA] amenusurika kifo baada ya gari lake kupinduka katika mlima kitonga wilaya ya kilolo kwenye barabara kuu ya Iringa -Dar es salaam.

Ajali hiyo imetokea mchana wa leo wakati gari hilo likiwa na watu wanne likitokea mkoani Mbeya kuelekea Dar es salaam,na hakuna aliyepoteza maisha katika ajali hiyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Ramadhan\ Mungi amethibitisha kutokea kwa ajari hiyo japo amesema taarifa kamili itatolewa na askari polisi waliokwenda katika tukio hilo la ajali.

0 comments:

Chapisha Maoni