Jumapili, Desemba 28, 2014

Vanessa Mdee akifurahia tuzo ya msanii bora wa kike Afrika Mashariki.

Mtangazaji/Msanii Vanessa Mdee na  Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ wamewakilisha vizuri Tanzania kwa kushinda tuzo zingine kubwa Nigeria za AFRIMA.

Vanessa ameshinda tuzo ya Best Female Artist in East Africa (Msanii bora wa kike Afrika Mashariki ) huku Diamond akishinda Tuzo Ya Best Male Artist in East Africa (Msanii bora wa kiume Africa Mashariki) . Tuzo ya Diamond ilipokelewa na Peter Msechu ambaye pia alikuwa kwenye kuwania tuzo hizo.

Peter Msechu,Vanessa Mdee na Victoria Kimani wakiwa na nyuso za furaha.

Peter Msechu baada ya kumpokelea tuzo Diamond Platinumz.

Hongera kwao na Peter Msechu kwa kuwakilisha vizuri.

0 comments:

Chapisha Maoni