Ijumaa, Desemba 12, 2014

JAMBO limezua jambo! Mapigano ya wakulima na wafugaji wa jamii ya kimasai yaliyotokea hivi karibuni katika Kitongoji cha Dumila, Wilaya ya Kilosa mkoani hapa yamewakurupua wazinzi waliokuwa wakifanya uchafu wao katika nyumba ya kulala wageni.

Mwanahabari wetu aliyenasa tukio hilo lililotokea Desemba 9, mwaka huu, alimshuhudia dereva wa lori ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja, akitoka katika gesti maarufu eneo la Dumila akiwa na nguo ya ndani huku binti aliyekuwa akibanjuka naye akikurupuka na taulo ambapo nguo zake za ndani na mazagazaga yake alicha chumbani.


 Binti akiwa ndani ya chumba cha gesti.

 Gesti iliyovunjwa vioo.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, mapigano hayo yaliyodumu kuanzia saa 4 asubuhi hadi 10 jioni, yaliibuka baada ya mmasai huyo kumkata mkono mkulima katika mashamba ya Kijiji cha Mteteni alipokuwa akimzuia kukata majani shambani kwake.

Chanzo hicho kilizidi kudai kuwa, baada ya wakulima kuona mwenzao amekatwa mkono, walijikusanya na kuwavamia wafugaji hao ili kulipa kisasi.

Nguo za ndani zilizoachwa.

“Wamasai baada ya kuzidiwa nguvu na kundi hilo la wakulima, waliamua kukimbilia msituni ambapo baada ya kuwakosa, wakulima hao waliamua kufunga barabara kuu ya Morogoro-Dodoma inayokatiza kwenye Kitongoji cha Dumila kushinikiza serikali ya wilaya, mkoa na taifa kuwaondoa wamasai kwenye wilaya yao,” kilieleza chanzo hicho.

Polisi wakiwa eneo la tukio.

Wakati hayo yakiendelea ndipo vijana wanaodhaniwa kuwa ni wa kutoka katika jamii ya wakulima walipoamua kuvamia gesti na nyumba za wamasai kisha kuvunja vioo vya madirisha na baadaye kuvunja mlango.

Vijana waliokamatwa na polisi.

Mbali na dereva wa lori na kiburudisho chake ambacho pia hakikujulikana jina lake kukurupuka katika gesti hiyo, mwandishi wetu alishuhudia wateja wengine wakitimka wakiwa watupu huku wengine wakiwa wameshikilia nguo za ndani mkononi.


crdt:GPL

Bofya hapa kujiunga nasi facebook ili upate taarifa mpya kila zinapotufikia 

0 comments:

Chapisha Maoni