Ijumaa, Machi 21, 2014

Ajali ya kutisha imetokea huko nchini Brazil leo majira ya saa 10:00am kwa saa za Afrika mashariki baada ya gari aina ya Toyota Hilux Pickup kupinduka katika barabara kuu ya state highway 010.

Kwa mujibu wa dereva wa gari hilo ambae aliomba ahifadhiwe jina lake alisema,ndani ya gari hilo kulikuwa na watu sita,dereva mmoja na wengine sita.

Dereva huyo aliendelea kunyetisha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi,ambapo dereva huyo alishindwa kulidhibiti gari hilo lilipodumbukia katika shimo kubwa lililokuwa katika barabara hiyo na kupinduka.

Majeruhi wote waliokolewa na kikosi cha zimamoto nchini humo na kupelekwa katika hospitali ya HPS Ana granddaughter iliyopo Pimenta Bueno nchini Brazil.

Alipohojiwa na polisi wa nchini humo alisema kuwa gari lilikuwa jipya na halikuwa na muda mrefu tangu liliponunuliwa kutoka dukani hivyo hakuwa bima (insurance).

Baadhi ya watu walioshuhudia ajali hiyo walimlaumu dereva huyo kwa kutembea mwendo kasi lakini pia pia waliilaumu serikali kwa kutozima mashimo mengi katika barabara hiyo kuu kwani hicho ndio chanzo kikubwa cha ajali nchini humo. 




0 comments:

Chapisha Maoni