Ijumaa, Machi 21, 2014

Shabani akiwa na vitenda kazi vyake akiwa eneo la kanisa.

Angalia picha za mtu aliyejitambulisha kwa jina la Shabani Hamisi alikuwa akijihusisha na vitendo vya kishirikina, akiwa chini ya wanamaombi wa kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha mara baada ya mtu huyo kukamatwa usiku wa kuamkia leo wakati wa maombi kanisani hapo ambapo ametoa maelezo mbalimbali namna alivyokuwa akishiriki katika vitendo hivyo vya kishirikina.

 Akiwa amevua shati huku akiwa anaombewa.

 Vitenda kazi vyake vikiwa vimemwagwa chini.

 Kazi kwelikweli.

Baadhi ya vitendea kazi vikiwa chini.

Katika hali isiyo ya kawaida mtu huyu ajulikanaye kwa jina la Shabani Hamis amenaswa akiwa anafanya uchawi katika kanisa la Ufufuo na Uzima Arusha.

Pamoja, na kukutwa bila nguo mtu huyo aliyekuwa amebeba vifaa ambavyo kwa mujibu wa maelezo yake, huvitumia kuwanga na kupaa ni pamoja na tunguli na kikapo cha mkoba wa uchawi. Tukio hilo la aina yake limetokea Usiku wa saa sita, wakati mkesha wa maombi ukiendelea kanisani hapo.

0 comments:

Chapisha Maoni