Jumatano, Januari 22, 2014


Watu wakitembea karibu na sanamu ya umbo inayojulikana kama 'Red Cube'  wakati tufani ya theluji ilpokua inaanza kuanguka New York "Jiji lisilolala" siku ya Jumanne January 21, 2014 na kusababisha nyuzi joto kushuka na kusababisha shule kufungwa yakiwemo maeneo mengi yakazi zikiwemo huduma za mabenki kwa ajili ya usalama wa wafanyakazi wao kuelekea nyumbani mapema kabla hali haijakuwa mbaya. Theluji iliyoanguka ilikuwa kati ya inchi 5 mpaka 10. 

Wapenzi wakitembea kwenye theluji iliyoanza kuanguka mitaa ya jiji lisilolala, New York siku ya Jumanne January 21, 2014, Theluji hiyo iliendelea kuanguka kwenye majimbo mengine yaliyopo ukanda huu wa kaskazini mashariki ya Marekani na kuleta baridi kali iliyosababisha theluji kuwa barafu iliyoleta adha kubwa kwa waendesha vyombo vya moto na viwanja vingi vya usafiri wa anga kusitisha safari.

Mdau akikatiza mitaa ya New York huku akipata kikombe cha kahawa kuongeza joto mwilini siku ya Jumanne January 21, 2014 wakati theluji ilipokua ikianza kuanguka kwenye jiji hilo lisilolala.

Sanamu ya Liberty  ikiwa haionekani kutokana na tufani hiyo ya theluji iliyoanguka kwenye mji huo wa New York siku ya Jumanne January 21, 2014. Theluji ilianza kuanguka kuanzia saa 4 asubuhi mpaka usiku wa manane na kuleta baridi kali.

Watu wakitembea mtaa wa Wall wa New York wakati wa tufani hiyo ya theluji ilpokuwa ikiendelea kuanguka siku ya Jumanne January 21, 2014.

Mpiga box akiwa na wakati mgumu wakujaribu kugawa vidonge kwenye tufani ya theluji iliyoanguka siku ya Jumanne January 21, 2014 na kuleta baridi kali iliyowapa wakati mgumu wakaazi wa mji huo wa jiji lisilolala.

0 comments:

Chapisha Maoni