Ijumaa, Januari 24, 2014


Tukio la kustaajabisha limetokea leo mchana nchini Brazil,ambapo vijana wawili walijaribu bahati yao katika kituo cha gesi na kuiba. Wakati wakijaribu kutoroka, mtu mmoja aliyekuwa jirani na kituo hicho cha gesi alimpiga risasi ya mgongo mmoja wa wezi hao.


Hata hivyo mwizi huyo alifanikiwa kupanda pikipiki tayari kwa kukimbia,lakini baadae alianguka umbali mchache kutoka pale alianguka na kufa hapohapo.

Mwizi mwenzake aliyekuwa nae,alifanya tukio lililoshangaza watu wote eneo hilo,alivyoona mwenzake amezidiwa alisimamisha pikipiki na kumshusha,bila yeye kujulikana alipoelekea. 







Polisi bado wanaendelea na uchunguzi juu ya tukio hili,ingawa taarifa za awali za jeshi la Polisi nchini humo zinasema wawili hao ni miongoni mwa wahalifu sugu wanaotafutwa kutokana na wizi wa aina hiyo katika maeneo tofauti ya nchi hiyo.


Kiongozi wa Polisi nchini humo alibeza tukio la wezi hao kama alivyonukuliwa akisema

 'I just love seeing the people getting fed up with crime and doing the police and judicial system’s job. No tax money to feed this moron in prison. I would throw his body in a sewer and present the rats with a late Christmas present'.

0 comments:

Chapisha Maoni