Jumamosi, Januari 25, 2014


 Chanel Tapper.
Chanel Tapper, mwanafunzi kutoka California, USA,amevunja rekodi ya kuwa na ulimi mrefu zaidi kuliko watu wote duniani.

Ulimi unagusa miwani.
Ulimi wake una urefu wa 9.75 cm ( sawa na 3.8 Inches.), kutoka ncha ya mdomo wa juu.Ulimi huo una urefu wa mara mbili ya urefu wa kawaida wa ulimi wa mwanadamu.

Mwanadada huyo alieleza kuwa "Wakati nikiwa na miaka nane,mimi na mama yangu tukijianda na Halloween (sikukuu ya watakatifu) ilibidi tupige picha ya ukumbusho,na miongoni mwa mapozi ya picha hizo ni kutoa ulimi nje,ndipo watu walipoanza kuushangaa ulimi wangu"

  Chanel Tapper akishindana ulimi na mwenzake.
Mwanadada huyo aliongeza kuwa
 "Mimi niliona ni kawaida tu ila kadri watu walivyokuwa wanatazama picha hizo na kuuzungumzia ulimi wangu nliona kabisa kuna utofauti,lakini mama alinipa moyo na kunambia ni hali ya utoto tu ambayo itaisha nikikua na nitakuwa na ulimi wa kawaida kama binadamu wengine,cha kushangaza mpaka sasa nimekuwa mkubwa na ulimi bado upo vilevile,siku hizi sichukii kama zamani watu wakinambia nina ulimi mrefu na nachukulia ni hali ya kawaida kabisa".

0 comments:

Chapisha Maoni