Jumatatu, Desemba 01, 2014

POLISI mjini Hong Kong nchini China na waandamanaji wanaodai demokrasia wamepambana katika eneo linalozunguka makao makuu ya serikali.

Ili kutuliza maandamano hayo, polisi wamelazimika kutumia maji ya pilipili huku wakiwa wamejihami kwa silaha ili kuwatawanya waandamanaji.

Takribani watu 48 wanashikiliwa na polisi kutokana na maandamano hayo ambayo yamechukua miezi miwili hadi sasa.

Madai ya waandamanaji hao ni kutaka kuwa na uhuru wa kuchagua viongozi wao bila kuingiliwa na Beijing.

Polisi wakielekea kuwakabili waandamanaji mjiini Hong Kong.

Polisi wakimtia nguvuni mmoja wa waandamanaji.

Mmoja wa waandamanaji akipewa kichapo na piolisi.

0 comments:

Chapisha Maoni