Jumanne, Desemba 09, 2014

HAUSIGELI aliyenaswa kwenye video akimtesa mtoto nchini Uganda, amefikishwa mahakamani.

Mfanyakazi huyo Jolly Tumuhirwe ameiambia mahakama kuwa anajutilia kile alichokifanya na anaomba msamaha.Ameshitakiwa kwa kosa la kumtesa mtoto Arnella.

Licha ya taarifa ya polisi kusema Jolly atashitakiwa kwa kosa la jaribio la mauaji, kiogozi wa mashitaka alimshitaki Jolly kwa kosa la kumtesa mtoto mdogo.

 Jolly Tumuhirwe akiwa mahakamani.

 Jolly Tumuhirwe alipokuwa akimtesa mtoto Arnella.

Bi.Tumuhirwe alikiri makosa yake na kuomba msamaha. Hakuna wakili yeyote aliyemwakilisha Jolly mahakamani licha ya mmoja wa mawakili mashuhuri kusema angemwakilisha Jolly bila malipo.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Jumatano ambapo hakimu anatarajiwa kutoa hukumu yake dhidi ya Jolly.

Huenda akafungwa jela miaka 15 au kutozwa faini ya dola mia nne au adhabu zote

0 comments:

Chapisha Maoni