Jumatatu, Machi 17, 2014

 Maiti ya mtu asiyefahamika imekutwa katika eneo la Foz do Iguaçu,pwani ya Paraná kusini mwa Brazil.huku maiti hiyo ikiwa imeharibika sana na baadhi ya maeneo ya mwili wa marehemu hiyo yakiwa hayawezi kutambuliwa vizuri kutokana na kuharibika.

 Maafisa wa jeshi la polisi wakichukua ushahidi.
 Jeshi la Polisi nchini Brazili lilipigiwa simu na wasamaria wema wanaoishi maeneo ya pwani ya mto wa Paraná huko kusini mwa Brazil na kuarifia kukutwa kwa mwili huo maeneo ya pwani hiyo.

 Baadhi ya maeneo yaliyopigwa risasi.
 Baada ya polisi kufika eneo la tukio walifanikiwa kukuta mwili huo ukiwa umeharibika sana,huku ukiwa na majeraha kadhaa ya risasi maeneo mbalimbali ya mwili huo.

Sehemu ya tumbo iliyochanwa na kuwekwa mawe ili mwili usielee.
Pia iliarifiwa kuwa wauaji hao wasiofahamika waliichana maiti hiyo maeneo ya tumboni na kujaza mawe mazito ili maiti hiyo isiweze kuelea juu ya maji kama njia pekee ya kuficha uhalifu wao.

Baadhi ya mawe hayo yalifanikiwa kutoka katika mwili huo na hivyo mwili huo kuweza kuelea kuonekana katika pwani hiyo ndipo wasamaria wema waliokuwa maeneo hayo waliweza kutoa taarifa kwa jeshi la polisi.

Jeshi la polisi nchini humo bado linaendelea na uchunguzi ili kuwagundua wauaji hao.

0 comments:

Chapisha Maoni