Alhamisi, Februari 06, 2014




 Askariwa Jeshi la Polisi wakiondoa Vizuizi vilivyokuwa Vimefunga Barabara.

Baadhi ya wananachi wa kijiji hicho wakimzonga mkuu wa Wilya ya Mvomero Anthony Mtaka [mwenye shat la damu ya mzee] huku mkuu wa polisi Wilaya ya Mvomero OCD ldd Abdallah lbrahim akimlinda
Wananchi hao walikamatwa wakidaiwa kuwapiga mawe polisi wakati walipofyatua magomu ya machozi

KWA mara nyingine tena leo mamia ya wakulima wamefunga barabara kuu ya Morogoro-Iringa Kijiji cha Mangae wilayani Mvomero  Mkoani hapa,baada ya kundi la wafugaji jamii ya Wamasai kuwavamia mashambani na kuwapiga wakulima  kilichosababisha kujeruhiwa vibaya wakulima watano.

Kwamijibu wa mashuhuda Amina Kitengule dada wa majeruhi Rashi Abdalah mwenye hali mbaya ambaye ni miongoni mwa majeruhi watano waliolazwa hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambaye anadaiwa kuharisha na kutapika Damu kutokana na kipigo hicho,alisema kaka yake huyo alikumbwa na mkasa huo jana jioni wakati akianda shmba lake msimu huu wa kilimo.

Amina alisema siku ya tukio wakulima wakiwa shamba lilitokea kundi la wafugaji jamii ya Wamasai wakiwa na aina mbalimbali za sialaha za jadi na kuanza kuwachapa wakulima hao waliokuwa mashmbani.

“sisi hapa tunalima katika kitongoji cha Mkangazi,kwa muda mrefu tumekuwa na tatizo hili la kuvamiwa na wafugaji na kupigwa kisha kujeruhiwa nakila tukitoa taarifa serikalini hazifanyiwi kazi”alisema Amina na kuongeza
“mfano jana jioni walitokea tena hao Masai na kumvamia kaka yangu akiwa analima,wakamny’ang’anya jembe na na kuanza kumpiga nalo kwenye makalio walipoona hawaridhiki na kipigo hicho wakaanza kumchoma na mkuki…sasa hivi anaharisha na kutapika damu hospitali ya mkoa”

Mbali na kupigwa Rashid Abdalah,inasadikiwa zaidi ya watu watano walipigwa katika maeneo tofauti na kujeruhiwa vibaya kwenye miili yao kabla hawajakimbizwa hospitali ya rufaa kwa matibabu.

Kufuatia kuenea kwa taarifa za wakulima hao kupigwa na wafugaji, kuanzia saa 2 asubuhi wakulima walijikusanya na kuamua kuziba barabara hiyo kwa lengo la kushinikiza mkuu wa mkoa Dk Joel Bendera kufika hapo kutatua mgogoro huo.

Kwa mujibu wa wakulima hao uamuzi wa kumwita mkuu huyo ni kutokana shutuma za kukithiri kwa rushwa kwa viongoizi wa wilaya hiyo jambo ambalo limekuwa linalea na kuukuza mgogoro huo sambamba na kuwatia hasara na vilema visivyo tarajiwa.

“hatufungui barabara mpaka mkuu wa mkoa aje maana hatuana imani tena na uongozi wote wa wilaya”walisikika wakisema baadhi ya wananchi hao muda mfupi baada ya mkuu wa wilaya na kamati ya ulinzi na usalama kufika eneo hilo.

 Akiwasihi kufungua barabara hiyo kwa madai kuwa atalishugulikia suala hilo kwa kuwakutanisha wakulima na wafugaji,Mkuu wa wilaya hiyo akiwa juu ya gari la polisi alisema kiliochao kimesikika na anaahidi kutafuta ufumbuzi mapema iwezekanavyo.

Hata hivyo wakulima hao walikataa kufungua barabara hiyo na kuendelea kuchochea moto kwa kumwagia mafuta ya petrol kwenye mataili ya magari yaliyokuwa yamepangwa barabarani.

Kufuatia kukaidi kwa agizo hilo na kuendelea kuchomwa moto mataili hayo,Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro,Faustine Shilogile alilazimika kufika eneo hilo na kuagiza polisi waliokuwa eneo hilo kuwatawanya kwa kupiga risasi za moto hewani.

Hata hivyo kama sia jajizi wakulima hao walikaidia na kuanza kuwapopoa kwa mawe polisi na viongozi waliokuwa eneo hilo jambo lililomlazimu Kamanda Shilogile kuagiza kupiga mabomu ya machozi yaliyosaidia kuwatawanya na kufunguliwa kwa barabara hiyo.

Juhudi za kuupata uongozi wa hospitali ya rufaa Morogoro juu ya majeruhi wa mapigano hayo hazikuweza kufanikiwa kutokana na uongozi huo kudaiwa kuwa nje kwa kazi za kiofisi.






0 comments:

Chapisha Maoni