Alhamisi, Februari 27, 2014

Mwaka jana ulizuka mzozo ama mjadala kati ya wadau wa muziki wa Bongo Flava kufuatia kauli za Diamond Platinumz kumtaja mara kwa mara Dully Sykes kama muanzilishi wa Bongo Flava.
September 16 mwaka jana, Diamond alishare picha kwenye Instagram akiwa na Dully Sykes na kuandika, “with the Bongo Flavour Founder, Legend of the Legends @princedullysykes…going back home.”

Kufuatia kauli hiyo, mtandao wa Bongo5 uliandika Makala ya kuiweka sawa kauli ya Diamond Platinumz ikiwa na data nyingi zinazohusu historia ya muziki wa Bongo Flava, ‘Diamond anamuita Dully Sykes muasisi wa Bongo Flava, well acha turefresh.’

Tovuti ya Times Fm imekutana na Prince Dully Sykes, pamoja na mambo mengine ilitaka kufahamu mtazamo wake kuhusu kauli ya Diamond Platinumz na kama yeye pia anadhani swaiba wake huyo hakuwa sahihi kwa mujibu wa historia ya muziki wa Bongo Flava.

Dully Sykes alisisitiza kuwa yeye ndiye muasisi/muanzilishi wa Bongo Flava akitoa sababu zake:
Yupo right na hajakosea, anaetaka kubishana…abishane na mimi. Mwaka 1999 mimi ndio nilizaa muziki wa kuimba Tanzania ambao ni Bongo Flava, ulikuwa unaitwa ‘Mwanasesele.’ 2001 ukaanza kupigwa vita muziki ambao mimi naimba. Nikaoneshwa kwamba naimba muziki ambao ni mwanasesele na sifanyi hardcore ambayo ni hip hop kufika platinum 5. Hakutajwa mwingine nikatajwa mimi, hakukuwa na mwanamuziki ambaye anaimba Tanzania zaidi yangu, wengine wote walikuwa wafa
 niliyeuza muziki wa kuimba ‘Bongo FLava’. 

Na mimi ndiye niliyezalisha wanamuziki wazuri wanaofanya vizuri mpaka leo. Akina Barnaba, akina Mr Blu akina Shetta, akina Mavoko, akina Diamond. Wote wametoka katika mikono yangu.
Bongo Flava ni yangu na hakuna mtu anakataa, nasemea Bongo Flava muziki wa kuimba. Bongo flava jina alitoa Steve B, Steve ndiye alitoa jina. Lakini mimi nilitoa muziki wenyewe halali wa kuimba Tanzania. 

Msikilize Dully kwa kubofya play hapa chini...

0 comments:

Chapisha Maoni