Jumatatu, Februari 17, 2014

 Leo February 17 kutoka Mhakama kuu kanda ya Dar es salaam,msanii wa maigizo nchini Tanzania Elizabeth Michael maarufu Lulu alikuwa akisomewa shitaka lake la kuua bila kukusudia msanii mwenzake wa maigizo Steven Kanumba April 07 2012  eneo la Vatican.

 Akisoma maelezo ya awali wakili wa serikali Monica Mbogo mbele ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo Rose Teemba amesema mshtakiwa siku ya tukio kulikuwa na ugomvi kati ya marehemu na mshtakiwa na baadaye mshtakiwa aliondoka usiku wa saa sita baada ya marehemu kuanguka chumbani ambapo alfajiri ya february 07  majira ya saa 11 alfajiri Lulu alikamatwa eneo la Bamaga.


  Kwa upande wake wakili  Peter Kibatala ambaye anamtetea Lulu amesema wameridhishwa na sehemu kubwa ya  maelezo ya awali ya mteja wao, ambapo kesi hiyo imeahirishwa mpaka itakapopangwa tena huku kila upande ukitarajia kuleta mashahidi watatu.


0 comments:

Chapisha Maoni