Jumamosi, Februari 01, 2014

Tembo akiwa amekufa katika moja ya Mbuga za wanyama nchini, huku meno yake yakiwa yameondolewa

Wakati Taifa likididimia katika umaskini wa kutisha, wanyama ambao ni kitega uchumi cha nchi wanauawa kila siku na kundi la watu wenye uchu wa fedha. 

Tanzania ni nchi ya pili Afrika kwa kuwa na idadi kubwa ya tembo, baada ya Botswana.

Hata hivyo, ripoti kutoka Taasisi ya Utafiti wa Wanyama Pori (Tawiri), inaonyesha kuwa tembo 30 wanauawa kila siku katika mbuga mbalimbali hapa nchini.

Tawiri inaeleza kuwa miaka ya 60, Tanzania ilikuwa na tembo kati ya 250,000 hadi 300,000, lakini mpaka kufikia mwaka 2011, kuna tembo 70,000.

Utafiti uliofanyika umebaini kuwa upotevu huu wa tembo, unafanywa na genge la maharamia wenye mtandao uliojisuka hadi serikalini.

0 comments:

Chapisha Maoni