Alhamisi, Januari 23, 2014

Mkuu wa Ushirikiano kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania Eric Beaume (kushoto) akibadilishana hati ya makubaliano ya Mradi wa Kupambana na Ukatili kwa Watoto  na Mwakilishi wa UNICEF hapa nchini Jama Gulaid, kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Plan International Tanzania Jorgen Haldorsen, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid na Mkurugenzi Mkazi wa Save the Children International Tanzania Steve Thome wakishuhudia makabidhiano ya hati hiyo jana jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Ushirikiano kutoka Umoja wa Nchi za Ulaya Tanzania Eric Beaume (kushoto) akipeana mkono na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid mara baada ya kumkabidhi hati ya makubaliano ya msaada kwa ajili ya Mradi wa Kutokomeza ukatili kwa watoto utakaotekelezwa kwa ushirikiano wa Serikali,UNICEF,Plan International na Save the Children, wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Plan International Tanzania Jorgen Haldorsen,na wa kwanza kulia ni Mwakilishi wa UNICEF hapa nchini Jama Gulaid,

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt Seif Rashid (aliyeko mstari wa mbele katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau wa Mradi wa kutokomeza Ukatili kwa Watoto mara baada ya kutia saini msaada kutoka Umoja wa nchi za Ulaya jana jijini Dar es Salaam.

0 comments:

Chapisha Maoni