Jumamosi, Januari 25, 2014


Shirikisho la Soka Afrika (CAF), limemuidhinisha mshambuliaji wa Yanga, Emmanuel Okwi, kuichezea klabu hiyo katika mashindano yao ya Klabu Bingwa Afrika, wanayotarajia kushiriki mwezi ujao.

Uamuzi wa CAF umetokana na kuridhishwa na vielelezo walivyotuma kwa ajili ya usajili wa michuano hiyo. Yanga wameweka wazi hati hiyo waliyotumiwa na CAF kuhusu kumruhusu Okwi kuichezea timu hiyo kwenye mashindano yao.


Kuidhinishwa kwa mshambuliaji huyo raia wa Uganda, aliyewahi kuchezea Simba, kabla ya kuuzwa katika timu ya Etoile du Sahel ya Tunisia, kumezidisha maswali magumu kwa wadau wa soka Tanzania, baada ya Jumatano iliyopita TFF kusimamisha usajili wake mpaka ipate ufafanuzi kutoka FIFA.

Akielezea uamuzi wa TFF kuhusu Okwi, Katibu Mkuu wa Yanga, Beno Njovu, amesema “Hii ni aibu kubwa, maana CAF wao wameona namna gani Okwi ni mali ya Yanga, hivyo TFF inapaswa kuwa makini katika hili, maana wameonyesha udhaifu mkubwa.”

0 comments:

Chapisha Maoni