Jumatatu, Januari 20, 2014

Wakati ambapo rais wa Ufaransa, Francois Hollande na First Lady, Valerie Trierweiler wanahangaika kuuweka sawa uhusiano wao kufuatia tuhuma za Hollande kuwa na uhusiano wa kimapenzi na muigizaji Julie Gayet, ndoa ya rais Barack Obama wa Marekani na Michelle nayo inadaiwa kuwa juu ya mawe.


Yote yalianza kwenye hafla ya kumbukumbu ya Nelson Mandela mwishoni mwa mwaka jana pale ambapo zilisambaa picha zinazomuonesha Michelle akionekana kukerwa na kitendo cha mumewe kupiga picha ya ‘selfie’ na Waziri Mkuu wa Denmark Helle Thorning-Schmidt.


Na kama magazeti ya udaku ya Marekani yanasema ukweli, uhusiano wa wawili hao upo kwenye matatizo makubwa.

Katika kichwa cha habari kisemacho: ‘Obama Divorce Bombshell’, gazeti la National Enquirer linadai kuwa ndoa hiyo yenye miaka 21 imekuwa ikikumbwa na ugomvi wa mara kwa mara ulioanzishwa na tukio hilo kwenye hafla ya kumbukumbu ya Mandela na mbaya zaidi ni kuwa Michelle amegundua kuwa walinzi wa Secret Service wamekuwa wakificha uzinzi unaofanywa na Obama.

Ni madai ambayo ikulu ya White House imegoma kusema chochote.

0 comments:

Chapisha Maoni