Jumamosi, Januari 24, 2015

NI fununu tu! Mwanamuziki wa kizazi kipya, Juma Jux, ameweka bayana kile kinachoendelea kati yake na Vanessa Mdee ‘V Money’ kuwa ni mambo ya kikazi na si uhusiano wa kimapenzi.

Msanii wa muziki wa RnB nchini Tanzania, Jux akipozi katika studio za Global TV Online.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Global TV Online, Jux aliyasema hayo kutokana na tetesi zilizokuwa zikiandikwa kwenye mitandao ya kijamii, kwamba amejiweka kwa mwanadada huyo anayetamba na Wimbo wa Siri alioshirikiana na Barnaba.

Jux akiwa kwenye pozi baada ya kufanya mahojiano.

“Ni fununu tu, hakuna jingine. Mimi na Vanessa tupo kikazi, nakumbuka nilipokuwa nataka kufanya video yangu ya Sisikii, nilikuwa natafuta msichana wa kuwa naye kwenye video, kwa sababu alikuwepo, basi hakukuwa na jinsi, nikaamua kumtumia kwani aliujua wimbo vizuri hivyo nikaamini kwamba video ingekuwa poa sana na kweli ikawa hivyo,” alisema Jux.

Baada ya mahojiano, Jux alipata fursa ya kupiga picha na wanahabari wa Global Publishers Ltd.

Bofya hapa chini kutazama video ya Jux akizungumzia ukweli kuhusu yeye na V-Money...



Crdt: GPL

0 comments:

Chapisha Maoni