Jumatano, Januari 28, 2015

Mwonekano wa lango kuu la Club ya Olympia baada ya kuungua.

Askari wa zima moto wakiwa kazini.

Sehemu ya ndani ya club hiyo ikionesha majivu ya vitu vilivyoungua.

 Askari wa zima moto wakiwa kwenye gari lao.

 Mashuhuda wa tukio wakitazama hasara iliyosababishwa na mto.

Askari wa zima moto wakinyoosha mipira ya maji.

CLUB Olympia iliyoko Sinza-Mori jijini Dar es Salaam, imeungua na kuteketea kwa moto majira ya saa kumi na nusu usiku wa kuamkia leo ambapo chanzo cha moto huo hakikuweza kufahamika mapema.

Mlinzi wa club hiyo inayomilikiwa na Samuel Mwaisumbe, na ambaye hakuweza kujitambulisha jina lake, alisema moto huo ulianza mishale ya saa kumi usiku ambapo waliweza kutoa taarifa kwa vyombo vya zima moto.

Aliongeza kwamba zima moto hawakufika kwa muda mwafaka na badala yake walifika kunako saa 12 asubuhi wakiwa na maji kidogo ambayo yaliisha wakati moto ukiendelea.

0 comments:

Chapisha Maoni