Jumanne, Desemba 02, 2014

UKATILI! Mwanamke mmoja, Regina Salago (24) (pichani) ameuawa kinyama kwa kupigwa na kitu kizito kichwani na kuvunjwavunjwa shingo na mikono na mume wake, Kishimba Keya, kutokana na wivu wa kimapenzi.

Tukio hilo la kinyama, limetokea hivi karibuni katika Kijiji cha Maganzo, Kata ya Songwa wilayani Kishapu, Shinyanga.Akizungumza na gazeti hili kuhusu tukio hilo, mama mzazi wa Regina aliyejitambulisha kwa jina la Catherine Kondo (45) alisema siku mbili kabla ya kifo, binti yake huyo alikuwa amerudi nyumbani kutoka kwa mumewe kwa nia ya kuachana naye. 

 Regina Salago enzi za uhai wake.

‘’Siku aliyorudi mwanangu aliniambia amechoshwa na vitendo vya wivu wa kupita kiasi anavyofanyiwa na mume wake, ameona bora arudi nyumbani aanze upya maisha akiwa huru hata kama ni ya shida,’’ alisema mama huyo. Aliongeza kuwa Regina alishinda siku mbili tu nyumbani hapo ndipo mume wake alimfuata na kumbembeleza kuwa waondoe tofauti zao na kwamba alikuwa amejirekebisha.


Bofya hapa kujiunga nasi facebook ili upate taarifa mpya kila zinapotufikia 

0 comments:

Chapisha Maoni