Alhamisi, Desemba 04, 2014

Askari polisi pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya mtaa kata ya Gongoni manispaa ya Tabora wakiangalia mwili wa mwanaume mmoja ambaye ni Msusi katika moja ya Saloon za wanawake hapa manispa ya Tabora inayofahamika kama HK,Mwanaume huyo ambaye amefahamika kwa jina la Ramadhani amekutwa amefariki dunia akiwa chumbani kwake katika nyumba ya kulala wageni inayofahamika kwa jina la SALAMA GUEST ambapo ilidaiwa kuwa alikuwa ameishi katika nyumba hiyo kwa muda wa siku tatu na hatimaye kufikwa na umauti.

Mwili ulichukuliwa na Polisi baada ya kuvunjwa mlango wa chumba katika Guest House hiyo. 

Dada huyu inasemekana kuwa ndiye alikuwa mpenzi wake marehemu huyo Ramadhani

0 comments:

Chapisha Maoni