Jumamosi, Desemba 06, 2014

 Leo tarehe 06/12/2014 itakuwa ni siku ya kihistoria kwa wanafunzi wa chuko kikuu cha sayansi na teknolojia Mbeya (MUST) baada ya serikali yao wa wanafunzi kuhakikisha wamekata kiu yao ya burudani.

Katika sherehe za kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka kwanza chuoni hapo zilizoanzia tangu asubuhi kwa kuwepo kwa mabonanza ya michezo mbalimbali katika viwanja tofauti tofauti vya michezo vilivyo chuoni hapo.

Katika shamrashamra za hafla hizo ilikuwepo session ya kupata brudani kutoka kwa Mrisho Mpoto almaarufu kama "Mjomba" ambae alikuwa hapo kutoa Inspirational speech kama kawaida yako iliyojitika zaidi katika kuwahamasisha wasomi wa uhandisi chuoni hapo kujijua wao ni akina nani na wana nafasi gani katika jamii.




 Mjomba akiwa amepozi baada ya kufika katika ukumbi wa Nyerere chuoni hapo.


 Mjomba akitafakari cha kuongea na wasomi wahandisi.
 Mjomba na wawakilishi wa serikali ya wanafunzi pamoja na uongozi wa chuo wakiingia ukumbini.
 Mjomba akimsikiliza kwa makini mshereheshaji.
 Raisi wa serikali ya wanafunzi MUSTSO akifungua sherehe hizo.

 Muwakilishi kutoka ofisi ya mshauri wa wanafunzi akitia neno.
 Naibu makamu mkuu wa chuo akisema chochote katika sherehe hizo.
 Mshereheshaji akimkaribisha Mrisho Mpoto "Mjomba".

 Mrisho Mpoto akishangaa baada ya kuonyeshwa upendo wa kutosha.

 Mjomba alianza makamuzi kwa kuonyesha uzalendo wa kuimbisha wimbo wa taifa.


 Mjomba akiimbisha wimbo wa taifa kwa hisia kali.
 Wimbo wa taifa ukiendelea.

 Wajumbe wakishangilia baada ya Mjomba kumaliza kuimbisha wimbo wa taifa.

 Mjomba baada ya kuanza makamuzi.


 Akiendelea kukamua...


 Akisisitiza jambo...

 Kama kawaida yake kutovaa viatu "Pekupeku"






 Akilonga na hadhira...







 Akiuliza lengo la kusoma la mwanafunzi mmojawapo



 Akiendelea kuchekesha...







 Akiendelea kufanya yake...






Mjomba alishukuru sana kupewa na nafasi hiyo iliyohudhuriwa pia na Naibu Makamu mkuu wa chuo hicho akimuwakilisha Makamu Mkuu wa chuo hicho Professor J.Msambichaka.

Miongoni mwa yale yaliyosemwa na mjomba kwa wanafunzi hao wa uhandisi ni
1.Kwanza watafute nafasi katika jamii zinazowazunguka
2.Watengeneze jina zuri katika jamii kutokana na kazi za mikono yao na
3.kutumia fursa walizo nazo katika kujiingizia kipato.

Bado sherehe zinaendelea kwenye viunga mbalimbali chuoni hapa..
Ni kazi yangu kuhakikishwa haupitwi na kila kinachoendelea hapa na kwingineko.
Endelea kufuatilia hapa ili uburudike zaidi....



0 comments:

Chapisha Maoni