Jumamosi, Desemba 27, 2014

Nguli wa sinema za Komedi Bongo, Amri Athuman ‘Majuto’ akiwa na Kajala Masanja.

NGULI wa sinema za Komedi Bongo, Amri Athuman ‘Majuto’ amefunguka kuwa, mastaa wengi wa kike wamemgeuza babu yao kwa kumfanyia vituko kila wanapokutana naye.

Akisema mbili tatu na paparazi wetu baada ya kusambazwa kwa picha mtandaoni inayomuonesha akifanyiwa vituko  na staa mwenzake, Kajala Masanja, Mzee Majuto alisema watu wasimfikirie ndivyo sivyo kwani yeye wasanii wengi wa kike wamemgeuza babu yao.

 Mzee Majuto akiwa na Odama.
“Wasanii wengi wamenizoea sana, huwa wananitania mara kwa mara na miye nawachukulia kama wanangu hasa hawa mastaa wa kike tofauti na wanaume, sijawahi kuwa na uhusiano na staa yeyote kati yao,” alisema Mzee Majuto.

0 comments:

Chapisha Maoni