Jumapili, Novemba 23, 2014

Ni habari ya kusikitisha sana kupata taarifa hizi kwa kila mwenye moyo wa binadamu. Mtoto huyu ambaye alioneshwa akiteswa na house girl katika video iliyorekodiwa kwa siri na camera iliyotegeshwa sebuleni bado yupo katika hali mbaya.

Mtoto alivunjika mbavu kutokana na kukanyagwa sehemu ya mbavu zake.

Hizi ni habari za kusikitisha sana mtoto mzuri kama huyu malaika asiye na makosa kunusurika kukatizwa maisha yake kwenye mazingira kama haya. Mwandishi wetu anazidi kusisitiza juu ya umakini kwa wazazi na walezi wote kuwa makini katika kuwafahamu vizuri watu wanaowaachia watu wanaowaachia majukumu ya kuwalea watoto wao. 

Ni vyema kujipatia uhakika juu ya tabia za wasaidizi hawa wanaofanya kazi ya kushinda na kulea watoto wetu wakati wote ambao tunakuwa katika majukumu mengine ya kila ili kuweza kuendesha maisha yetu.

Ni kweli kwamba hatuwezi kufanya haya majukumu wenyewe bila usaidizi wa mabinti wa kazi. Wao ni muhimu na msaada mkubwa katika kuhakikisha kwamba watoto wanabaki salama na shughuli nyinginezo zinaendelea kama kawaida katika kuendesha maisha ya yetu na familia kwa ujumla. 

Lakini imetupasa kuwa makini kutokana na matukio kadhaa ya ukatili wa jinsi hii kwa watoto. Ni vyema kujua kwa undani tabia na mazingia ambayo msaidizi huyu amelelewa na kukua, na kupafahamu mahali anapotokea na ndugu zake.




0 comments:

Chapisha Maoni