Jumatatu, Aprili 07, 2014

Madereva  wa  gari  la magazeti ya kampuni ya The Guardian Rashid Yusuph Kahese (37) kushoto na mwenzake Ally Malinda (44) ambao  wamenusurika katika utekaji huo.


 Gari la magazeti  la kampuni ya The Guardian ambalo  limetua  Iringa  hivi sasa saa 2.40 Asubuhi  hii  baada ya  kupona  kutekwa .

MAJAMBAZI  ambayo  idadi  yao haikufaanika  mara  moja  usiku  wa leo  wamefunga barabara  ya  Morogoro -Iringa eneo la Doma na  kufanya  unyama  wa  kutisha kwa  wasafiri  wa barabara  hiyo ikiwa ni pamoja na kuwalazimisha  kufanya mapenzi wanaume kwa wanaume na kuwatesa  vibaya  madereva kabla ya kuwapora mali  zao.

Miongoni  mwa  walioteswa na pamoja na rasta  dereva wa gari la magazeti ya kampuni ya  globalpublishers ambae anadaiwa  kujeruhiwa mkono  wake  huku  dereva wa gari la magazeti ya kampuni ya Mwananchi akinusurika na gari lake   kupinduka wakati  akikwepa vizuizi  vya magogo  vilivyotegwa  barabarani.

Wakizungumza na mtandao  huu asubuhi ya  leo mjini Iringa  wahanga  wa  tukio hilo Ally Malinda (44) mkazi wa Itunda  Dar es Salaam na Rashid Yusuph Kahese (37) mkazi wa Mbezi jijini Dar es Salaam  ambao  kwa  pamoja  wanaendesha  gari ya magazeti ya kampuni ya The Guardian walisema  kuwa  tukio  hilo  lilmetokea  mida ya saa 8  usiku wa leo  hadi saa 11 Alfajiri  baada ya watekaji hao kuachia  mateka hao .

Malinda  alisema kuwa  kabla ya  kufika  eneo ambalo  watekaji  hao  walikuwa  wamewateka  abiria  wengi zaidi  walikutana na makundi  ya  watu  waliotekwa  na  kuporwa ambao  walikuwa  wakiwasimamisha  wasiendelee na  safari  ila  hawakusimama  wakijua ni  wezi .

" Tulienda  mbele  kidogo  tukakutana na kundi  jingine ila  bado tulipuuza na kupita baada ya  kufika mbele  ndipo  tuliona magari  yakiwa  yamegeuka  huku na kule  huku  wengine  wakiteswa  na ndipo  tulipofanikiwa kugeuza gari  letu lenye namba za usajili T 812 CNZ na  kukimbia  .

Hata  hivyo alisema  polisi  Morogoro  walipigiwa simu  ila hawakuweza kufika hadi majira ya saa 11 Alfajiri  watekaji hao  walipoamua  kuwaachia mateka.

" Kila  tukimpigia kamanda wa  polisi mkoa wa Morogoro aliishia  kusema kuna askari  wametumwa kuja  eneo la tukio ila hadi asubuhi hakuna askari  aliyefika .....na majeruhi  wamepelekwa  Hospital ya mkoa  wa Morogoro kwa matibabu zaidi"

Mtandao  huu unaendelea  kumtafuta  kamanda wa  polisi wa mkoa wa Morogoro  ili kuzungumzia  tukio hilo  zaidi .

0 comments:

Chapisha Maoni