Jumapili, Aprili 06, 2014

 Ajali hii ilitokea usiku wa kuamkia  leo jumamosi  katika daraja la mto Kanoni barabara iendayo Bandarini kwenye manispaa ya Bukoba, Gari hiyo ndogo aina ya  Toyota yenye namba za usajili T910 CTC, ambalo mmiliki wake hajajulikana.

Japo katika eneo la tukio mwananchi mmoja alisikika akisema ni mali ya Askari Polisi ambae hakumtaja jina, Mtandao huu ulifika kwenye kituo cha Polisi kujiridhisha na tulikutana na Bw Magayane ambae ni msaidizi katika kitengo cha Usalama Barabarani alikiri kuwa na Tarifa za ajali hiyo na kusibitisha kuwa hakuna aliyeumia, na nilipotaka kujua mmiliki wa Gari hili alisema hawamjui wapo katika jitihada za kumtambua.



Wananchi wakiangalia ajali ya gari  Daraja la mto Kanoni barabara iendayo Kastam bandarini.


 Namba za usajili za gari hiyo.





Ushauri: Ulevi na matumizi ya simu uwapo barabarani ni hatari.



0 comments:

Chapisha Maoni