Jumatano, Aprili 23, 2014

 Picha ya chini na juu ni baadhi ya majeruhi walikuwa kwenye  basi hilo aina ya Urio lililopata ajali leo jioni katika eneo la Kia wilayani Hai  mkoani Kilimanjaro.

 Wananchi wakiwa wanashuhudia ajali hiyo iliotokea leo jioni katika eneo la kia ambapo inasemekana watu zaidi ya 31 wamejeruhiwa.


Basi aina ya Urio yenye namba za usajili T 137 BCX inayofanya safari zake moshi kuelekea  leguruki mkoani  Arusha leo limepinduka katika eneo la kia na kujeruhi watu zaidi ya 31

Kwa mujibu wa mashuhuda waliokuwepo katika eneo la tukio walisema kuwa dereva huyo alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki iliyokuwa imejichomeka barabarani

"dereva huyu alikuwa anajaribu kukwepa pikipiki ndipo gari ikamshinda na kuama barabara ndipo ilipo anguka gafla  na kubiringita mara tatu apa yenyewe unavyoiyona tumeigeza ilikuwa kichwa chini matairi juu"alisema mmoja wapo wa shuhuda ambaye hakutaka kujitambulisha jina.

mpaka kamera yetu inaondoka eneo la tukio watu 31 walikuwa wamekwishwa pelekwa katika hospitali ya wilaya ya hai kwa ajili ya matibabu wakiwemo wanafunzi wa shule ya leguruki ambao walikuwa wanarejea shuleni mara baada ya kumaliza likizo yao ya sikukuu ya pasaka .

0 comments:

Chapisha Maoni