Ijumaa, Machi 07, 2014

 Wahamiaji Haramu hao walikamatwa juzi katika kitongoji cha Gezaurole katika kata ya Ruaha Mbuyuni tarafa ya Mahenge wakati jeshi la polisi likiwa katika doria ya kawaida na kulitilia mashaka gari hilo lililokuwa limebeba matenga ya Nyanya.

  Kiongozi wa Wahamiaji Haramu,akiwagawia wenzake mikate  ilionunuliwa na wanahabari waliokuwepo kwenye tukio hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi mkoani humo.

  Kiongozi wa Wahamiaji Haramu,akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusiana na sakata lao la kukamatwa nchini Tanzania,anasema wamesafiri nchini kwao Ethiopia mpaka Tanzania kwa siku 21



 Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi akizungumza na Waaandishi wa habari mapema leo mchana,kwenye makao ya Polisi ya mkoani humo,akithibisha kukamatwa kwa wahamiaji haramu hao wakiwa katika roli lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga wakitokea nchini Ethiopia kuelekea nchini Afrika Kusini.

  Roli lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga ndilo lililotumika kuwabeba wahamiaji hao.

  Matenga ya Nyanya ambamo Wahamiaji hao walikuwa wamekaa.

JESHI la Polisi mkoa wa Iringa limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 46 kutoka Ethiopia waliokuwa wakielekea nchini Afrika ya Kusini.

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Iringa ACP Ramadhani Mungi amethibitisha kukamatwa wahamiaji hao wakiwa katika roli lenye usajili wa namba T 342 AJU likiwa linaendeshwa na dereva Mbega Ally (37) mkazi Tanga..

Mungi alisema wahamiaji hao walikamatwa juzi katika kitongoji cha Gezaurole katika kata ya Ruaha Mbuyuni tarafa ya Mahenge wakati jeshi la polisi likiwa katika doria ya kawaida na kulitilia mashaka gari hilo.

“Jeshi la polisi lilipata habari za kiintelejensia kuwa kuna roli limebeba wahamiaji haramu vijana wakajipanga na kufanikiwa kuwakamata wakiwa katikakati matenga ya nyanya yaliyopangwa kwa pembeni na na kufanikiwa kuwakamata vijana hao 46 akiwemo mtoto wa miaka 17” alisema Mungi.

Alisema kuwa dereva wa gari hilo anashikiriwa na jeshi la polisi kwa mahojiano zaidi na kusema baadhi ya Waethiopia hao 6 kati yao wana hati ya kusafiria (passport).

Katika hali kuonyesha ukarimu kwa wageni hao haramu waandishi wa habari walioko katika kampeni za jimbo la Kalenga wa mkoa wa Iringa na nje ya mkoa waliwapatia msaada wa vyakula wahamiaji hao baada ya kuonyesha wanakabiliwa na njaa kali na kiu ya maji.

Waandishi hao wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa Iringa (IPC), Frank Leonard walichangishana na kupatikana kiasi cha shilingi elfu 50 na kufanikiwa kuwapatia vyakula hivyo.

0 comments:

Chapisha Maoni