Ijumaa, Machi 07, 2014

Hii imetokea Marekani ambapo mama huyu mwenye umri wa miaka 32 akiwa ni mjamzito, aliamua kuliendesha gari hili na kuliingiza kwenye bahari kwa makusudi huku watoto wake wakipiga kelele kwamba mama anajaribu kutuua.

Watoto wa Mwanamke huyu ambae imeripotiwa kwamba bado yuko hospitali akifanyiwa vipimo vya matatizo ya akili, ambao wana umri wa miaka mitatu, tisa na 10 walichukuliwa na Idara ya watoto na familia kwenye jimbo la Florida baada ya kupata matibabu.

Watoto hawa wote walikuwemo kwenye gari hili lililolengeshwa baharini na mama yao ambae anadai alikua anakwenda kwenye sehemu salama ambayo mume wake walieachana asingeweza kuwafata au kujua waliko.

Wakati hili tukio linatokea alikuepo karibu Mtalii raia wa Canada ndio maana video ya tukio na hizi picha zimepatikana zikionyesha kila kitu.

 Huyu ni miongoni mwa watu waliojitokeza kuokoa baada ya kusikia kelele za mtoto aliyekua ndani ya gari akisema ‘mama yetu anatuua’

Bofya play kuangalia video hapa chini...
 

0 comments:

Chapisha Maoni