Ijumaa, Machi 07, 2014

Mtu mmoja amekufa papo hapo na wengine 22 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la kampuni ya saibaba walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya kupinduka katika kijiji cha Mwambegele wilayani Rungwe.

Safari ya basi la kampuni ya Saibaba lenye namba za usajili T 973 AVW kutoka jijini Dar es Salaam kwenda wilayani Kyela imeishia kwenye kona kali ya Mwambegele wilayani Rungwe, baada ya basi hilo kupinduka, ambapo mkuu wa wilaya Rungwe Crispine Meela ni miongoni mwa watu ambao wamewahi kufika kwenye eneo la tukio na hapa anaelezea chanzo cha ajali hiyo.

Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo ambao wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Rungwe, makandana, wamesema mwendo kasi wa basi hilo ndio ambao umewasababishia ajali ambayo imesababisha kifo cha dereva wa basi hilo.

Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Rungwe, Mandana, Stanford Mwakatage amethibitisha kupokea mwili wa mtu mmoja na majeruhi 22 wa ajali hiyo huku akisema kuwa baadhi ya majeruhi hali zao bado sio za kuridhisha.

Bofya play kuangalia taarifa hiyo...

0 comments:

Chapisha Maoni