Jumapili, Machi 02, 2014


Kijana aliyejulikana kwa jina la Almir José Nunes mwenye umri wa miaka 17,mkazi wa Pernambuco huko nchini Brazil,amekutwa amekufa katika barabara ijulikanayo kama Sítio Massapé,katika mji wa  Altinho,Pernambuco, Brazil.

Kabla ya kifo chake Marehemu Almir José Nunes,alikuwa akilalamikiwa sana katika jiji la Pernambuco nchini Brazil kwa wizi wa vifaa vya electronic na mifugo ya wakazi wa maeneo hayo.

Jeshi la Polisi nchini Brazil limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ingawa walishindwa kutoa kauli ya haraka ya nini kilisababisha kifo chake na ni nani aliyeondoa baadhi ya viungo vya marehemu huyo,lakini ilidhaniwa kuwa ni wanyama wakali kutokana na ushahidi wa kimazingira uliokutwa eneo hilo.

Bado jeshi la polisi nchini humo linaendelea na uchunguzi kugundua ni nani aliyefanya shambulizi hilo na kusababisha kifo hicho.

Tazama picha zaidi hapa chini...

 Mwili wa kijana Almir José Nunes.

 Mashuhuda wa tukio wakiuangalia mwili wa marehemu Almir José Nunes.

 Baba mzazi wa marehemu Almir José Nunes.
 Uso wa marehemu Almir José Nunes unavyoonekana.
 Muonekano wa eneo la tukio.
 Mwili wa marehemu Almir José Nunes.
 Majeraha aliyayoyapata mkononi.
 Marehemu Almir José Nunes enzi za uhai wake.


0 comments:

Chapisha Maoni