Jumatano, Februari 26, 2014

 Tiwonge Chimbalanga (kulia) na Steven Monjeza.
WIKI moja baada ya mwanamuziki wa kike wa Marekani kufanikisha kuachiliwa huru kutoka gerezani kwa mashoga wawili wa Malawi ambao walikamatwa na kuhukumiwa kwa kufanya ushoga, Steven Monjeza amemwacha Tiwonge Chimbalanga na kwenda kuoa mwanamke.

Steven aliviambia vyombo vya habari kwamba alikuwa amechoka na uhasama uliokuwa unamkabili si kutoka katika jamii tu, bali kutoka kwa familia yake pia na ameamua kuachana kabisa na ushoga.

"Nimechoka. Nililazimishwa kuingia katika ufuska huo na ninajuta. Nataka kuishi maisha ya kawaida... si maisha ambayo kila mtu atanitazama, kunicheka na kunizomea."
Steven Monjeza (kushoto) akiwa na Tiwonge Chimbalanga siku ya harusi yao.
Hivi sasa ameanza uhusiano na msichana mwenye umri wa miaka 24 kutoka mjini Blantyre. Na Tiwonge bado ana msimamo wa kumpenda Steven, akisema kwamba mwenza wake huyo wa zamani ameamua kuchukua mwanamke kwa ajili ya "kumuumiza roho".

Aliongeza kusema: "Lakini sina wasiwasi. Huwezi kulazimisha penzi, kwani hakuna mtu aliyemlazimisha tulipofunga ndoa yetu ya kihistoria mwezi Desemba.... Bado nitaolewa kwani kuna wanaume wengi wazuri. Nitaendelea kuwa shoga."

0 comments:

Chapisha Maoni