Jumapili, Februari 02, 2014

Manchester City kwenye uwanja wao wa Etihad. Hawa jamaa balaa sana kwenye uwanja wao msimu huu. 
Kwenye mechi 11 za Ligi Kuu England walizocheza uwanjani hapo msimu huu wamefunga mabao 42.

Kocha Jose Mourinho, Jumatatu atasafari na kikosi chake cha Chelsea kwenda uwanjani hapo, lakini tayari ana wasiwasi wa kupigwa tano au sita.

Arsenal, Tottenham na West Ham kila moja zilifungwa mabao sita zilipokwenda Etihad msimu huu, Norwich City ilipigwa saba na Manchester United ilikung'utwa mabao manne.

Kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, CSKA Moscow na Viktoria Plzen zilikubali kuruhusu mabao tisa kwenye nyavu zao zilipoifuata Manchester City nyumbani. Etihad si mahali pazuri kabisa kwa wapinzani msimu huu. Mourinho atapaweza?

Vinara hao wa Ligi Kuu England wanaonolewa na Manuel Pellegrini walianza msimu kwa kusuasua baada ya kupokea vichapo kutoka kwa Cardiff City, Aston Villa, Chelsea na Sunderland na pia kutoka sare dhidi ya Stoke na Southampton, lakini rekodi ya kwenye uwanja wao wa nyumbani inatisha.

Nani ataweza kuwadhibiti? Chelsea itakwenda uwanjani hapo ikiwa na kumbukumbu ya ushindi wa mchezo wao wa mzunguko wa kwanza, lakini hilo linaweza kuwa baya zaidi kama Pellegrini atahitaji kulipa kisasi.

Manchester City itamkosa straika wake, Sergio Aguero, lakini bado wana mastraika wengine hatari zaidi, Alvaro Negredo, Stevan Jovetic, Eden Dzeko, ambao wote ni hatari sana. Pellegrini watu wake muhimu kikosini anapocheza mechi kubwa ni Vincent Kompany, Samir Nasri, David Silva, Yaya Toure, Fernandinho, Gael Clichy na Zabaleta.

0 comments:

Chapisha Maoni