Raia wa Uganda akiwa aameshika bango, tayari kwa kushiriki katika maandamano ya kupinga sheria iliyowekwa ya kuvaa nguo fupi.
Kampala.Serikali ya Norway imesitisha msaada wa kiasi cha Sh 20 bilioni kwa Uganda baada ya Serikali ya nchi hiyo ya Afrika Mashariki kusaini muswada wa sheria dhidi ya ndoa za jinsia moja.
Sheria hiyo iliwaudhi viongozi wa nchi za Magharibi, ikiwamo Marekani, ambayo Rais wake, Barack Obama alieleza kuwa inafaa kuangaliwa upya.
Rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa mpinzani mkubwa wa vitendo vya ushoga, alisaini sheria hiyo Jumatatu wiki hii.
“Sheria hii mpya inapinga haki za msingi za binadamu na pia inakiuka katiba ya nchi hiyo (Uganda),’’ alisema Waziri wa Mambo ya Nje wa Norway, Borge Brende.
Aliongeza: “Tutazuia msaada wa Kroner 50 milioni (Sh 20 bilioni za Uganda) na tutaongeza jitihada zetu na nguvu zote na ushirikiano katika masuala ya haki za binadamu na kuhakikisha demokrasia inalindwa nchini Uganda.
Waziri huyo alitoa tamko hilo kupitia kwa msaidizi wa Balozi wa Norway nchini Uganda, Kyree Holm
“Rais (Museveni) alisaini muswada huo ambao unatoa adhabu kali kwa mtu yeyote atakayekutwa na hatia ya kufanya vitendo vya uhusiano wa jinsia moja, sheria ambayo inakiuka misingi ya raia wa nchi yake,” alisema Holm.
Naye Mkurugenzi wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya (EU), Catherine Ashton alisema kwamba kilichofanyika Uganda ni ubabe kwani huwezi kutoa kifungo cha maisha kwa kuwa na uhusiano wa jinsia moja.
Muswada wa kupiga marufuku uhusiano wa watu wa jinsia moja ulipitishwa Desemba mwaka jana na Bunge la Uganda baada ya mjadala mkali.
Miongoni mwa vipengele vya muswada huo, ni vile vinavyotoa amri ya kufungwa jela maisha kwa mtu atakayekutwa na hatia ya kuwa na uhusiano huo, ikiwa ni pamoja na wale wanaohamasisha na vitendo hivyo.
Hata hivyo, nchi za Magharibi ikiwamo Marekani zilikasirishwa na hatua hiyo ya Uganda.
Rais Obama alitishia kuwa uhusiano wa Uganda na nchi yake utaharibika kutokana na hatua ya Rais Museveni kusaini muswada huo na kuufanya kuwa sheria.
Muungano wa vyama vya wapenzi wa jinsia moja nchini Uganda umeazimia kuandaa sala ya pamoja ambayo wameiita ya amani ya kuiombea dua Serikali ya nchi yao baada ya kupitisha muswada huo kuwa sheria

0 comments:
Chapisha Maoni