Jumamosi, Februari 08, 2014

 Nyama ya nguruwe. Ugonjwa wa homa ya nguruwe, umeibuka tena katika Jiji la Mbeya na kuua nguruwe 166 wenye thamani ya Sh33 milioni hadi ilipofika juzi.

Ugonjwa wa homa ya nguruwe, umeibuka tena katika Jiji la Mbeya na kuua nguruwe 166 wenye thamani ya Sh33 milioni hadi ilipofika juzi.Tayari Mganga Mkuu wa Mifugo katika jijini hilo, Dk James Kawamala ametangaza karantini ya kuzuia kuingia au kutoa nguruwe kwenda katika eneo lingine.

Kwa mujibu wa matangazo yaliyobandikwa katika maeneo mbalimbali ya Jiji, ni marufuku kwa mtu yeyote kuchinja ama kusambaza na hata kutoa zawadi ya nyama ya nguruwe ambaye haijathibitishwa na daktari wa mifugo wa jiji.Alipoulizwa kuhusu hali ya ugonjwa huo, mganga huyo alisema ni mbaya na kwamba tayari nguruwe 166 wamekufa hadi juzi.

Alisema taarifa zinasema ugonjwa huo pia umeripotiwa katika Wilaya za Rungwe na Mbeya Vijijini.‘’Kwa namna yoyote ile, wanyama wote wa jamii ya nguruwe kwa sasa watatakiwa kuthibitishwa kwa kuliwa katika machinjio zilizopo jijini hapa,’’ alisema.

Ugonjwa wa homa ya nguruwe kwa mara ya kwanza ulizuka mkoani Mbeya mwaka 2011 ambapo nguruwe wengi walikufa na watu kupata hasara.

Kwa mujibu wa Dk Kawamala, Jiji la Mbeya, pekee ilipoteza nguruwe zaidi ya 1,500.

0 comments:

Chapisha Maoni