Alhamisi, Februari 27, 2014

Video ya wimbo wa KATY PERRY‘DARK HORSE’akiwa amemshirikisha JUICY J, imekumbwa na msala baada ya taasisi ya dini ya kiislam ya uibgereza inayojulikana kama SHAZAD IQBAL kutaka video hiyo iondolewe YOUTUBE kwa madai ya kumkashifu Mwenyezi Mungu.

Taasisi hiyo imedai kuwa kipande cha video hiyo kinachomuonesha mtu akiwa amevaa cheni iliyoandikwa ‘Allah’ yaani Mungu, akishindwa na nguvu za giza (Magic Power) za Katy Perryaliyetamba kuzitumia kwenye wimbo wake. Lakini kibaya zaidi katika dakika ya kwanza na sekunde kumi na tano ya video hiyo, mtu huyo anaonekana akichomwa moto na kuuawa.
Taasisi hiyo imeiandikia ‘petition’ YouTube na tayari maombi hayo yameshakusanya sahihi zaidi ya 40,000 kwenye mtandao. 

Bofya play hapo chini kutazama video hiyo....

0 comments:

Chapisha Maoni