Anasema alipoufungua alikutana uso kwa uso na fedha nyingi zaidi ya dila milioni moja za Singapore na papo hapo akaamua kuzipeleka katika ofisi ya serikali inayohusika na vitu vilivyopotea na kuzisajili zikisubiri atakayeulizia.
Katika mahojiano na gazeti moja dereva huyo alipoulizwa kwa nini hakuingia mitini na fedha hizo, alijibu kuwa kwanza pesa sio muhimu kwangi, pili pesa hizo sio za kwangu , akahoji kwanini nizichukue?
Inasemekana kuwa wale wapenzi watalii walitoa taarifa ya kupotelewa na mzigo wao katika kampuni inayomiliki taxi anayoendesha mzee Sia.
Haikuchukua muda taratibu zilifanyika kisha wakakabidhiwa kitita chao bila kupungua hata sumni.
Taarifa zinasema dereva huyo amezawadiwa na kampuni yake ya taxi hizo na atakabidhiwa tuzo ya heshima kwa uaminifu wake. Hata hivyo haijajulikana kampuni hiyo itampa zawadi gani.