Jumatano, Februari 05, 2014

BASI la Zuberi lenye namba T119 AA2 limepata ajali mbaya katika kijiji cha Nkuhi wilaya ya Ikungi Mkoa wa Singida na watu wanne wameripotiwa kufa papo hapo kwa kukatwa vichwa huku majeruhi wengi wakiwa wameumia vibaya sehemu mbalimbali za mwili.

Akizungumza na paparazi wetu kutoka eneo la tukio leo mchana,shuhuda wa tukio hilo alisema basi hilo la Zuberi lilikuwa linatoka Mwanza kuja Dar likiwa na zaidi ya abiria 60.

Amesema kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa basi hilo alikuwa anajaribu kumkwepa bibi kizee aliyekuwa anakatisha barabarani kwenye majira ya saa saba mchana.

“ilikuwa si ajali ya kawaida baada ya bibi kizee kukatiza barabarani na wakati dereva anajaribu kumkwepa alirudi mara ya pili barabarani ndipo hapo gari lilipinduka na kuanguka kwenye mtaro,” amesema Limu

Alilisitiza kwamba mashuhuda wa ajali hiyo wanahusisha tukio hilo na imani za kishirikiana baada ya bibi huyo kuamua kurudi mara ya pili barabarani na kusababisha ajali na kukaa kwa muda mrefu eneo la tukio.

Amesema kwa basi hilo la Zuberi liliinuliwa na lori lenye kifaa maalumu cha winch baada ya basi hilo kumlalia mtoto mdogo wa miezi kadhaa ambaye mama yake ni miongoni mwa waliofariki dunia papo hapo na maiti yake kupelekwa hospitali ya mkoa wa Singida.

0 comments:

Chapisha Maoni