Jumapili, Januari 26, 2014


Vijana wawili wa kibrazil wasiotambulika wameonekana ufukweni mwa bahari wakiwa wamebaki mafuvu tu baada ya kuliwa na samaki.


Vijana hao wenye umri unaokadiriwa kuwa kati ya miaka kumi na minane mpaka ishirini na tano inasemekana walikuwa wakiogelea katika ufukwe huo na kuelekea kina kirefu kujiburudisha,cha ajabu ni kutoonekana kwao kwa kipindi kirefu mpaka zilipokutwa maiti zao katika ufukwe huo wakiwa wameharibiwa vibaya baada ya kuliwa na samaki.


Kuna uwezekano kuwa wameng'atwa na samaki ajulikanae kama piranhas kwa jinsi miili yao ilivyo,alisema mmoja wa wavuvi wa eneo hilo.

 Samaki wanaosemekana kuwala vijana hao.

 Mmoja wa miili ya vijana hao.
Mvuvi huyo aliongeza kuwa,kwa jinsi nimjuavyo samaki huyo angewala na kuwamaliza wote ila kubaki kwa sehemu ya viwiliwili vyao ni dalili tosha kuwa aidha waliwahi kuonekana katika fukwe hizo au nyama za mwili wao zilikuwa zimewahi kuharibika kitu ambacho samaki hao hawapendelei sana.


0 comments:

Chapisha Maoni