Ijumaa, Januari 31, 2014

Watu watatu akiwemo dereva wa gari ndogo aina ya Ford fiesta nyeusi na wanawake wawili wamepoteza maisha katika ajali mbaya iliyo usisha  gari ndogo aina ya Ford fiesta nyeusi na lori aina ya mercedes 1318.

Tukio hili ambalo limetokea katika mji wa Crateus jimbo la kaskazini mashariki nchini Brazili liliripotiwa kuwa ndani ya gari hiyo ya Ford fiesta kulikuwa na watu watano.
Lori hilo ambalo liligonga  gari hilo dogo kwa upande wa kushoto lilisababisha dereva na wanawake wawili walio kuwa wamekaa siti ya nyuma ya gari hilo kupoteza maisha
.
Wakati tukio hili linatokea vijana wengine wawili kati ya hao watano walijeruhiwa vibaya na huku wale waliokuwa katika lori wakitoka salama bila kupatwa na majeraha.
Baada ya kutokea kwa ajali  hiyo dereva wa lori hilo aliwaita watu wa huduma ya kwanza katika eneo la tukio kwaajili ya kutoka msaada.
Polisi walipo fika katika eneo la tukio waliwachukua majeruhi pamoja na dereva wa lori hilo kwaajili uchunguzi zaidi.

ANGALIA PICHA ZAIDI ZA AJALI HIYO
 



0 comments:

Chapisha Maoni