Alhamisi, Januari 23, 2014


 Elisante Saidi (51) mkazi wa kijiji cha Nduamughangawilaya ya Singida, akiwa amelazwa katika hospitali ya mkoa mjini Singida,baada ya kukatwa katwa Mapanga na kuchomwa Mkuki wa watu wanaodaiwa ni wakazi wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba mkoa wa Dodoma.Wakazi hao wa Nduamughanga, inadaiwa walikuwa wanataka kuwakomboa Ng’ombe wao zaidi ya mia moja waliokamatwa baada ya kuingia kinyume na sheria kwenye pori la akiba la Mgori.

 Nesi wa wodi namba tatu katika hospitali ya mkoa mjini Singida, Elionora Matayi akieleza juu ya kumpokea majeruhi Elisante Saidi aliyenusurika kuuawa na wakazi wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba mkoa wa Dodoma,ambao walikuwa wanataka kuwakomboa kwa nguvu Ng’ombe wao zaidi ya mia moja waliokamatwa baada ya kuingia kwenye hifadhi ya pori la Mgori.

 Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP,Geofrey Kamwela, akitoa taarifa kwa waandishi wa habari iliyohusu mhudumu wa wanyapori kijiji cha Nduamughanga wilaya ya Singida, kuuawa kwa kukakatwa mapanga kwenye ugomvi wa kugombea Ng’ombe zaidi ya mia moja.Ng’ombe hao mali ya wakazi wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba mkoa wa Dodoma,walikamatwa baada ya kuingia kwenye hifadhi ya msitu wa Mgori.

 .Ni baada ya mifugo kukamatwa kwa kosa la kuvamia hifadhi.
.Watumia nguvu kuvamia hifadhi ili kuchukua mifugo yao kibabe
Na Nathaniel Limu, Singida

WATU wasiojulikana idadi yao wakazi wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba Mkoani Dodoma, wamemuua mhudumu wa wanyamapori, Athumani Jumanne (40) kutoka cha kijiji cha Nduamughanga kwa kumkatakata mapanga sehemu zake mbalimbali za mwili.
Kifo cha Athumani inadaiwa kinatokanana kukatwa katwa mapanga kichwani na kupigwa mshale mdomoni.

Inadaiwa kuwa mauaji hayo yanatokana na ugomvi wa kugombea ng’ombe 180 wa wakazi wa kijiji cha Handa wilaya ya Nchemba mkoani Dodoma.

Inasemekana walikamatwa na mhudumu wa wanyamapori baada ya kuingia isivyo halali kwenye hifadhi ya akiba yam situ wa Mgori.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida, Geodfrey Kamwela amesema kuwa Athumani ameuawa januari 21 mwaka huu saa saba na nusu huko katika kijiji cha Nduamughanga kata ya Mughanga tarafa ya Mgori wilaya ya Singida.

Amesema siku ya tukio,kundi kubwa la wakazi wa kijiji cha Handa,waliingia katika kijiji cha Nduamughanga wakisaka kuwakomboa ng’ombe wao 180 waliokamatwa kwa kosa la kuingia ndani ya akiba ya hifadhi ya msitu wa Magori.

Akifafanua,Kamwela amesema uchunguzi wa awali unaonyesha wazi kuwa chanzo cha mauaji hayo ni ugomvi wa kugombea ng’ombe hao 180 waliokamatwa baada ya kuingia kwenye hifadhi ya akiba ya pori la Mgori.

“Wengi wa watu hao wamewahi kuvamia na kuishi katika eneo la akiba ya hifadhi ya msitu wa Mgori.Kutokana na kuishi kwa muda mrefu kwenye eneo hilo na baadaye kutolewa kwa nguvu,walikuja wakiwa na orodha ya majina ya watu ambao walitarajia kuwauawa”,amesema.
Kamanda huyo amesema kuwa baada ya kuvamia kijiji hicho cha Nduamughanga,waliweza kuwajeruhi Hamisi Ramadhani (36),Elisante Saidi (51),Omari Omari (42),Muna Hamisi (38) na afisa mtendaji wa kijiji cha Nduamughanga Mwaftari Rajabu (35).

Alitaja wengine kuwa ni Abrahamu Mhamed(60),Hnis Rajabu (33),Yohana Saidi (37),Ramadhani Rajabu (26),Msafiri Juma,Omari Hamisi (33),Hamisi Sharifu (32),Jumanne Hasani ,Abdi Musa,Daudi Karata,Helena Bakari (65) na Jumanne Musa (28).

“Majeruhi hao wote isipokuwa Elisante Said,waliweza kupatiwa matibabu katika zahanati ya kijiji cha Nduamughanga na kuruhusiwa kuondoka.Elisante yeye amehamishiwa katika hospitali ya mkoa iliyopo mjini hapa,na bado anaendelea na matibabu kutokana na kuumizwa vibaya”,amesema kamanda huyo.

Amesema kundi hilo baada ya kujeruhi watu hao 17,waliweza kumsaka mhudumu wa wanyamapori Athumani na walipompata,walimkata kata mapanga kichwani na kumpiga mshale mdomoni na kusababisha kifo chake papo hapo.

Kamanda Kamwela amesema kuwa baada ya hapo,walianza kusaka mahali ng’ombe wao wamehifadhiwa ili waweze kuwachukua kwa nguvu.

“Hawakuweza kuwapata ng’ombe wao 180 na badala yake walipora ng’ombe 68,mbuzi 101,kondoo sita na punda watatu mali ya Abrahamani Mohammed (60) waliokuwa wakichungwa mbugani,na kuondoka nao”,amesema Kamwela.

Amesema hadi sasa wamefanikiwa kuwakamata Nicodemo Ako (45) mkazi wa kijiji cha Giting wlaya ya Hanang mkoa wa Manyara na Athumani Soa (62) mkulima na mkazi wa kijiji cha Handa.Baada ya kumaliza uchunguzi,watu hao wawili watafikishwa mahakamani.

0 comments:

Chapisha Maoni