Jumatatu, Januari 20, 2014


ILE Oparesheni Fichua Maovu (OFM) chini ya Global Publishers, safari hii iko kimataifa zaidi ambapo wiki iliyopita ilitua huko Hong Kong, China na kunasa ufuska wa wanawake wa Kibongo wanaokwenda nchini humo kwa kigezo cha biashara kumbe wanakwenda kuuza miili.


Baadhi ya mastaa wa Bongo wakikata mauno nchini China.

OFM ilipata taarifa kutoka kwa chanzo chake ndipo ikatuma kachero wake nchini humo na kujionea vitu vinavyochafua taswira ya Tanzania nje ya nchi hasa China kama wanadada hao wanavyofanya uchafu tena wengi wao Bongo ni mastaa.


Wabongo wakijiachia nchini China.

“Kiukweli ni aibu! Wanawake wa Kibongo wanachezewa makalio hovyo, wanafanya vitendo vya ngono hadharani kwa ujira wa dolari za Kimarekani mia tu.

“Kuna msanii wa Bongo muvi aliyefulia ambaye ni mke wa mtu (mcheza soka wa kimataifa) hadi sasa yupo China, nimemuona kwa macho yangu klabu akichezewa makalio kwa dola mia moja,” alisema OFM wetu.


Wabongo wakiwa viwanja vya kujiuza nchini China.

Uchunguzi wa OFM ulibaini kwamba kuna makundi ya wanawake wa Kibongo wanaokwenda China wakijifanya wafanyabiashara lakini wengi wao hubebeshwa madawa ya kulevya ‘punda’ kisha huwa hawataki kurudi Bongo huku kukiwa na wengine wanaokwenda maalum kwa kujiuza.





Ijumaa Wikienda liliwasiliana na staa wa Kibongo aishie nchini humo, Rehema Fabian ambaye ni Mshiriki wa Miss Kiswahili 2009 ambaye alikiri kuwepo kwa mastaa na wabongo wengi wanaojiuza nchini humo.

Alipotafutwa Balozi wa Tanzania nchini humo, Abraham Shimo ili kupata undani wa ishu hiyo, simu yake ya ofisini ilikuwa ikiita bila kupokelewa hivyo juhudi za kumpata zinaendelea.

0 comments:

Chapisha Maoni