Jumanne, Januari 21, 2014


WAKATI  wanaharakati  mbali  mbali wakiwemo  wanaharakati  wa mtandao wa kijinsia  Tanzania (TGNP)  ,wanaharakati  wa  haki za binadam,WAMA kuendelea  kukemea na kuendelea  kupinga vikali vitendo vya  ukatili wa kijinsia na uyanyasaji wa  wanawake na watoto hata kulifanya jeshi la jeshi la  polisi  kuanzisha dawati maalum  linaloshughulikia vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia ,baba  wa kambo Mussa Mdetela aamua kuwatesa kinyama watoto wake kwa kuwachoma moto miguu  wakituhumiwa kuiba Tsh 10,000
Hivi  ndivyo  watoto  hao  walivyougunzwa  kinyama na baba wa kambo.

 Askari  wanaharakati  wa dawati la mtandao wa jinsia kulia na kushoto wakiwa  wamemkamata mama wa watoto  hao tayari kwenda polisi.
 
 Hapa wakiingia na mama  huyo katika ofisi za dawati la jinsia mkoa wa Iringa.

 Mrakibu mwandamizi  wa  polisi na mkuu  wa dawati la jinsia na  watoto mkoa  wa Iringa ,Atupele Mwambunda  akiwatazama  watoto hao nje ya ofisi ya  dawati la jinsia mkoa  wa Iringa.

 Askari  polisi akimuongoza mama  wa watoto hao polisi.
.
Mama  wa  watoto hao  Watende  Sanga  akiendelea  kupika chakula baada ya  watoto kuchukuliwa na polisi.

Askari  wa dawati la jinsia  Iringa akiingia kumsimamia  mama wa watoto hao kufunga duka lake kabla ya kuchukuliwa kwenda  polisi.

Wakizungumza  kwa shida na mtandao  huu  watoto hao Baraka Rajab Mohamed anayesoma darasa la kwanza na Mood Rajab Mohamed   anayesoma  darasa la sita walisema kuwa  ilikuwa ni siku ya tarehe 3 ambapo walichukua pesa hiyo kiasi cha Tsh 10,000 na kwenda kununua chakula baada ya  mama yao kushindwa kuwaandalia chakula.

Hata  hivyo Mood anayesoma darasa la sita  msingi Lugalo  alisema kuwa siku ya  tukio mdogo  wake  alikwenda ndani na kuchukua  kiasi hicho cha fedha na baada ya muda  walishirikiana katika matumizi .

Watoto  hao ambao wanadai kuwa baba  yao mzazi  Rajab Mohamed aliwaacha na sasa anaishi  jijini Dar es Salaam na wao  wamekuwa  wakiishi na baba yao mdogo huyo ambae  mara kwa mara amekuwa  akiwaadhibu vikali.
Kwani  walisema  kuwa kutokana na mara kwa mara kushinda bila kula ndipo siku  hiyo walipoamua kuchukua pesa  hiyo ili kununua bagia na vitumbua ili kujikimu kwa njaa .

Hata  hivyo  walisema baada ya  baba yao kurudi kutoka katika shughuli zake na kubaini kuwa  fedha  hiyo imechukuliwa ndipo alipowakamata na kuwafunga kamba na kuanza kuwatesa kwa kichapo ili waweze  kusema mtu aliyechukua pesa  hiyo.

“Alitufunga kamba miguuni na mikononi na kuanza kututesa kwa kutupiga na baada ya kuona hatusemi ndipo alipochukua makaratasi ya naironi na kutufunga miguuni kisha kuchukua kiberiti ,mafuta ya taa na kuwasha  moto katika miguu yetu huku akiendelea  kutupiga na moto ukiwaka miguuni….wakati huo mama alikuwa amekaa mlangoni akishangilia kuwa wapige sana mimi  nimewachoka hawa watoto heri wafe tu” walisema watoto hao

Atupele Mwambunda mkuu wa dawati la jinsia mkoa  wa Iringa ameuthibitishia mtandao  huu juu ya tukio  hilo na kuwa kitendo hicho ni cha kinyama na kamwe hakitavumilika.

Alisema kuwa  kuanzishwa kwa dawati hilo ni kutaka kukomesha  vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kama  hivyo na kuwataka  wazazi na jamii kuepuka kuchukua sheria mkononi kwa  kuwatesa  watoto kama hao ambao mwisho  wa  siku  wanapoteza mwelekeo wa maisha.

Mwambunda  alisema  kuwa hadi sasa wamefanikiwa  kumkamata mama  wa watoto hao Watende  Sanga huku  mzazi  mwenzake Mussa Mdetele bado anatafutwa  na jeshi la  polisi ili  kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za kuwatesa  watoto hao.

Huku mama  wa watoto hao  akidai  kuwa wakati baba yao mdogo akiwapiga watoto hao yeye hakujua kinachotokea  japo alikuwa na taarifa ya  kupotea kwa  pesa katika duka na kuwa baada ya tukio hilo aliwanunulia dawa ili kuwatibu  kinyemela pamoja na kuwaombea  ruhusa shuleni .

Pia mwanamke  huyo aliomba  kusamehewa kwa madai  kuwa hakujua kama kushangilia wakati  baba yao akiwatesa  watoto hao ni kosa.




0 comments:

Chapisha Maoni