Jumanne, Januari 21, 2014

MTOTO mmoja aliyetambulishwa kwa jina la Joyce Jeremia, 11,(pichani) amejeruhiwa vib
aya katika mapigano ya wa kulima na Wamasai ambao ni wafugaji katika Kijini cha Laitini, Kiteto mkoani Manyara.

Baba mdogo wa mtoto huyo Amos Njelu aliwasimulia waandishi wetu akiwa katika Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu (Moi) amesema kuwa mtoto huyo alijeruhiwa Jumamosi ya Januari 12, 2014 katika kijiji hicho ambacho kilivamiwa na wafugaji wa Kimasai.

Aliongeza kusema kuwa baada ya uvamizi huo Wamasai hao walichoma nyuma ambayo wazazi na watoto akiwemo yeye walikuwa akiishi lakini Wamasai hao waliweza kufanya mashambulizi na kumuaa baba yake na kumjeruhi mama yake huku akiona.

“Nilijaribu kumasaidia lakini nikakatwa panga kichwani na mama naye alikatwa mdomo na kukimbia kusikojulikana.

“Hadi hivi leo sina mawasiliano na mama yangu ambaye alikimbia na wadogo zangu wawili  ambao ni Furaha na Peter,” alisema mtoto huyo.

Mtoto huyo ambaye alipatwa na jeraha kubwa la kichwa amelazwa  Moi  katika Wodi ya watoto na 8 akiendelea  na matibabu huku akisaidiwa  na baba yake mdogo pamoja na shangazi yake.

Baba mdogo wa mtoto huyo alisema kuwa lengo la Wamasai hao lilikuwa ni  kuwaondoa wakulima hao ili waweze kuweka mifugo yao kwa ajili ya kuchungia.


Aliongeza kusema kuwa alikuwa anapata taarifa kutoka kwa majirani kuwa kaka yake aliyemtaja kwa jina la Kisuligwe Chilongola amefariki dunia kutokana na vurugu za Wamasai.

Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, ACP Akili Mpwapwa alikiri kuwepo kwa mapigano hayo ya wakulima na wafugaji.

“Ni kweli mauaji yalitokea hadi sasa idadi ya waliouawa ni kumi na majeruhi mmoja lakini kuhusu mtoto huyo hatukuwa na taarifa zake… tunaendelea na uchunguzi ,” alisema Kamanda Mpwapwa.

0 comments:

Chapisha Maoni