Jumatano, Januari 29, 2014

 KATIBU wa siasa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Nape Nnauye, akisikiliza kwa makini maswali ya waandishi wa habari, leo mkoani Mbeya.

 KATIBU wa siasa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Nape Nnauye, akifafanua jambo mbele ya waandishi wa habari mkoani Mbeya. AMESEMA KUWA CCM INALETA AFYA WATANI WAO WANALETA CHAFYA, WAKIFANYA MAANDAMANO.

 Mbunge viti maalum mkoa wa Mbeya. Dr. Mary Mwanjelwa(CCM), akiwa nje ya ofisi ya katika wa CCM Mkoa wa Mbeya.

KATIBU wa siasa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM), Nape Nnauye, amesema moja ya magamba yaliyovuka katika chama hicho ni pamoja na aliyekuwa Mbunge wa Jimbo  la Igunga, Rostam Aziz.

Ameyasema hayo leo tarehe 29/01/2014 alipokuwa akijibu maswali ya waandishi wa habari mkoani Mbeya, baada ya kueleza ujio wa Rais Jakaya Kikwete mkoani hapa kwa ajili ya kuazimisha miaka 37 ya CCM.

Alisema anakiri kuwa chama hicho hakipo sawasawa asilimia mia moja lakini sawa na nyumba iliyopasuka ukutani hivyo uwezekano wa kukarabati ni mkubwa kuliko ingepasuka mpaka kwenye msingi.

Alipoulizwa kuwa uongozi wa chama hicho unafuta historia ya chama chao kwa kusherehehekea kuzaliwa kwake tarehe ambayo hakikuzaliwa, alisema siyo mara ya kwanza kufanya hivyo.

‘’Tutaazimisha Februari 2, mwaka huu ili kuwapa nafasi hata wafanyakazi kuweza kuudhuria maandamano ya mshikamano yatakayoongozwa na Rais Kikwete wala siyo kufuta historia’’ alisema Nape Nnauye.

Alisema tayari viongozi wa chama hicho wameanza kuwasili mkoani Mbeya ambapo Februari 2, mwaka huu watafanya maandamano kutoka eneo la Soweto mpaka ofisi za CCM Mkoa, kisha wataelekea uwanja wa Sokoine.

‘’Sherehe zetu zitaambatana na shughuli za kijamii ikiwemo kujenga zahanati, kupanda miti maeneo ya vyanzo vya maji na zitaoneshwa na vituo vitatu vya luninga na kutangazwa na redio’’alisema Nape.

Alipotakiwa kujibu maswali kuhusu minyukano ya malumbano kwenye vyombo vya habari kwa wanachama na viongozi wao, alisema kuwa kila mtu anao uhuru wa kuzungumza lolote.

Alisema maswali mengine ataomba ayajibu Februari 3, mwaka huu yakiwemo kuhusu mambo waliyomshauri Rais Kikwete kuhusu mawaziri waliosema kuwa ni mizigo.

“Hivi kati yenu nani anayejua tulichomshauri Rais kuhusu Mmawaziri hao? Kama yupo anyoshe kidole, maana suala la ushauri ni siri hivyo naombeni maswali mengine nitayajibu tarehe. 

0 comments:

Chapisha Maoni