OPARESHENI ya Polisi wa Mkoa wa Morogoro na kikosi maalum cha kufichua Maovu (OFM), imemnasa mwanamke mjamzito katika kamatakamata ya machangudoa.
Polisi akimkagua changudoa mwenye mimba aliyenaswa akijiuza.
Katika oparesheni hiyo ya aina yake
iliyofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika eneo la Msamvu (Kambi
ya Itigi), wanawake 30 waliodaiwa kujihusisha na biashara hiyo
walikamatwa.
Waandishi wetu wakiwa na askari wa mkoa huo walimnasa mjamzito huyo anayedaiwa kuwa na mimba ya miezi sita akiwa mawindoni eneo hilo.
Mara baada ya mjazito huyo kukamatwa
alitoa yake ya moyoni kwa kusema kwamba anafanya biashara hiyo ili
kupata fedha za kujikimu na ujauzito wake haumpi shida yoyote.
“Jamani natafuta pesa za kujikimu na
maisha hapa mjini sasa mnatukamata tukale wapi? Hii mimba ni yangu na
ninayefanya ukahaba ni mimi niacheni,” alisema mdada huyo.
Pamoja na maneno yake, polisi walimbeba msobemsobe na kumfikisha kituoni pamoja na makahaba wengine....
0 comments:
Chapisha Maoni