Jumatatu, Januari 27, 2014


KATIKA HALI ISIYO YA KAWAIDA maiti ya mtoto mchanga imekutwa imetupwa katika eneo la kuhifadhia taka "jalala" huko Mbagala Nzasa A, maiti ya kichanga hicho ilikutwa ikiwa inatoa harufu huku mwili wake ukiwa umeharibika vibaya kutokana na kuliwa na wadudu.

'Mwandishi wetu akiwa katika eneo la tukio alishuhudia maiti ya kichanga hicho ikiwa imefungwa katika kanga yenye rangi nyeupe na bluu huku idadi kubwa ya Nzi ikiwa inazonga maiti hiyo huku ikiwa imeharibika vibaya sana', mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo akiongea kwa masikitiko makubwa alidai kuwa siyo mara ya kwanza tukio hilo kutokea katika eneo hilo kwani miaka miwili nyuma tukio kama hili liliwahi kutokea na mhusika alikamatwa baada ya uchunguzi wa kina uliofanywa na polisi wakisaidiana na raia wema.

Naye mjumbe wa eneo hilo Bwana Saidi Kitambulio alishangazwa na kutokea kwa tukio hilo la kustaajabisha na kulaani vikali ambapo mpaka tunatoka eneo la tukio walikubaliana na wananchi wa eneo hilo kuripoti kutokea kwa eneo hilo katika kituo cha polisi cha jirani ambapo jeshi la polisi litaendelea na utaratibu wake wa kawaida wa kumtafuta muhalifu aliyemtupa mtoto huyo eneo hilo.

Angalia picha za tukio hilo hapa chini....TAHADHARI PICHA ZINATISHA...



 











0 comments:

Chapisha Maoni