Alhamisi, Januari 23, 2014

CP HamdanMkurugenzi Mtendaji wa Huduma za Kipolisi wa Interpol Bw. Jean-michel Louboutin kushoto akimkabidhi Kamishna wa Polisi Zanzibar CP. Hamdam Omari Makame nembo maalum ya Interpool,

SHIRIKISHO la Polisi wa Kimataifa Duniani INTERPOL, limesema litaendelea kuunga mkono juhudi zozote zinazochukuliwa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha na kudumisha hali ya usalama wa Visiwa vya Zanzibar kwa lengo la kuimarisha utalii kwenye eneo hilo.
 
Ahadi hiyo imetolewa na Mkurugenzi  Mtendaji wa Huduma za Kipolisi wa Interpol Bw. Jean-michel Louboutin, wakati alipokutana na Kamishna wa Polisi Zanzibar CP Hamdani Omari Makame,  aliyetembelea Makao Makuu ya Shirikisho hilo mjini Lyon Ufaransa ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kiusalama yanayoigusa Zanzibar kwenye ukanda wa Afrika Mashariki.

Bw. Jean-michel amesema ipo haja kwa jumuia nyingine za kimataifa kuunga mkono juhudi za Tanzania katika suala zima la kuimarisha usalama wa eneo hilo lenye historia inayovuta watalii kutoka katika mataifa mbalimbali.

Katika ziara hiyo ambayo ililenga kuimarisha usalama wa kikanda, Kamishna Hamdani alisema kuwa Jeshi la Polisi nchini Tanzania litaendelea kutoa msukumo na kushirikiana na Interpol ili kusaidia katika mapambano ya uhalifu wa kimataifa.
Kamishna Handani ameutaja uhalifu ambao ni kero na kikwazocha uchumi kuwa ni pamoja na Ugaidi, Uharamia, Biashara haramu ya dawa za kulevya na uhalifu mwingine unaovuka mipaka.

Kamishna Hamdani ambaye amekabidhiwa nembo maalum ya Interol, pia alipata fursa ya kutembelea vitengo mbalimbali vya Makao makuu ya Interpol na kupatiwa muhtasari wa mafunzo yanayotolewa na Interol katika kuwajengea uwezo wa kiutendaji Maafisa na Askari wa kada mbalimbali.

0 comments:

Chapisha Maoni