Jumatatu, Januari 27, 2014

Sir Alex Ferguson.
Sir Alex Ferguson anaamini bado Manchester United ina nafasi ya kutetea ubingwa wake wa Ligi Kuu.
Klabu hiyo ya Old Trafford ipo nafasi ya saba kwa sasa wakiwa nyuma kwa pointi 14 kwa vinara wa ligi Arsenal ukiwa imebakia michezo 16.

Lakini Ferguson, ambaye amestaafu kuifundisha United Mei mwaka jana, amesisitiza kuwa mabingwa hao bado wanaweza kutetea taji hilo.

"Sijaifuta timu yoyote katika mbio hizi," alisema kocha huyo mwenye miaka 72 na kuongeza kuwa United ya sasa inayofundishwa na David Moyes, itakuwa bora zaidi katika kipindi hiki kilichobakia cha msimu.

Ferguson alizipongeza timu sita za juu yaani Arsenal, Manchester City, Chelsea, Spurs, Everton na Liverpool, lakini alisema United bado "ipo nyuma yao katika mbio hizo".

Vigogo hao wa Old Trafford wakiwa na mwenendo wa kusuasua tangu Moyes alipochukua jukumu la kuifundisha timu hiyo wakiondolewa katika Kombe la FA na Kombe la Ligi, japokuwa wamefuzu kirahisi kwa 16 bora ya Ligi ya Mabingwa.

United pia imefungwa mara tatu mfululuzo kwa mara ya kwanza tangu 2001 wakati waliponyukwa katika siku saba za kwanza za Januari, wakilala mbele ya Tottenham, Swansea na Sunderland.

Pia kwa sasa wapo nyuma kwa pointi sita kwa Liverpool inayoshika nafasi ya nne hivyo wapo kwenye uwezekano wa kukosa kucheza Ligi ya Mabingwa kwa mara ya kwanza tangu 1992.

Ferguson alisema: "Napata wakati mgumu kuingia nne bora, Napata wakati mgumu zaidi kusema nani atanyakuwa ubingwa wa ligi."
Moyes amefuzu mara moja kucheza Ligi ya Mabingwa akiwa na Everton pale 2005, lakini alitolewa na Villarreal katika mechi za mtoano.

Moyes mwenye miaka 50, alichukua jukumu la kuifundisha United baada ya kukaa miaka 11 ndani ya Goodison Park kabla ya Ferguson kumteua kama mrithi wake Old Trafford.

0 comments:

Chapisha Maoni